JINSI YA KUACHA KUTUMIA DAWA NA KUWA ASILI (NATURAL)

Hili ni swali ambalo watu wengi wenye nywele zenye dawa wamekua wakiuliza; Je nifanye nini ili nywele zangu ziwe za asili?. Leo tuangalie njia kuu mbili ambaxo unaweza kutumia ili kurudi kuwa natural (kuacha kabisa kutumia dawa ya nywele). Pia tutaangalia na hasara na hasara ya kila njia maana faida yake  zote in general ni kupata  nywele natural.

NJIA YA KWANZA
1.TRANSITION METHOD
Hiki ni kitendo cha kuacha dawa / matumizi ya dawa za nywele na kuruhusu ikue yenyewe huku ukikata (au kutrim) kidogo kidogo nywele za juu mpaka  utakapimaliza nywele zote zenye  dawa.

FAIDA YA TRANSITION 
🧚‍♀️Unapata  muda wa kuisoma nywele yako vizuri
🧚‍♀️Kama haupo huru na nywele fupi unabaki na nywele zako ndefu
🧚‍♀️Hausubiri kukua kwa nywele
🧚‍♀️Wakati wa transition unamuda wa kustyle na kusuka nywele zako upendavyo

 HASARA ZA TRANSITION
🧚‍♀️Texture ya nywele inakua tofauti
🧚‍♀️Process  ya transition inachukua muda mrefu kuliko kuzikata kabisa
🧚‍♀️ Nywele kukatika ni lazima na huwezi kueluka;  Kwani nywele yenye dawa zina heat  na chemical   damage hivyo ni lazima zitoke tu.

VITU VYA KUZINGATIA KIPINDI HIKI
🧚‍♀️Katika kipindi hiki ni lazima KUEPUKA  na wala KUJARIBU kutumia moto hotcombs na blow dryers vile vile usipige  pasi nywele zako utaharibu za chini zinazopelekwa kuwa natural.
🧚‍♀️Acha kabisa  kutumia bidhaa zenye viambata sumu especially SULFATES  NA PARABENS 🧚‍♀️PROTECTIVE style; Fanya protective style kupunguza manyanyaso ya kila siku kwako personally (maumivu ya kuchana nywele na kuzitreat) pia kwa nywele kusumbuliwa sumbuliwa kila siku. Protective style ni mitindo ambayo unaweza kufanya na kukaa nayo atleast siku 5 au zaid bila kuchana.
🧚‍♀️ kumoisturize (kuzipa unyevu)  nywele zako
🧚‍♀️ TRIM ncha mbovu mara kwa mara vizuri zaidi ni   baada ya miezi 2 au zaid ili kuondoa split ends (ncha zilizochoka) - Unatumia mkasi ila sio wa nguo.

NB: Pale nywele za asili zinaporefuka na kukutana na za dawa  ndipo kazi itaanza maana  Hii sehemu huwa ni  dhaifu sana Jitahid kufanya deep conditioner (steaming kwa lugha iliyozoeleka) kila  wiki ili kulinda na kuzipa nguvu nywele.

NJIA YA PILI
2. BIG CHOP (BC)
 Hii ni kwa wale wanaotaka kuwa na nywele  natural kuanzia mwanzo sasa wanakata nywele zote za dawa na kubaki na nywele  vifupi - TWA (teeny weeny Afro). In general in KUNYOA tu.

 FAIDA ZA BIG CHOP
🧚‍♀️Hausubiri  muda mrefu kuanza kuzitunza nywele zako kiusahihi
🧚‍♀️Unaanza fresh kabisa  bila dawa
🧚‍♀️Unakua na uwezo wa kujua aina ya nywele zako haraka na hivyo itakua rahisi kuzihudumia.

HASARA ZA BIG CHOP
🧚‍♀️Unasubiri kidogo ili  nywele zikue
🧚‍♀️Unatakiwa  uitambue nywele yako haraka
🧚‍♀️Inaanza  na style mpya ya kuwa na nywele fupi.

BUT: Yote ni maamuzi yako  angalia ipi itakua njia sahihi kwako.
La muhimu zakdi ni  KUEPUKA  MATUMIZ YA MOTO WA AINA YOYOTE ILE KWENYE NYWELE.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad