VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA UKIWA KWENYE TRANSITION PERIOD

Hizi ni tips/mambo muhimu mtu anavyotaikiwa  kufanya akiwa kwenye transition yaani kutoka nywele yenye dawa kwenda nywele natural bila kufanya big chop (bila kukata nywele zote).

🧚‍♀️Usiweke  dawa tena kuruhusu nywele ziotee
🧚‍♀️ Punguza matumizi ya moto au usitumie kabisa.
🧚‍♀️Zingatia sana kufanya pre poo
NB: Fanya  pre_poo kabla ya kuosha nywele kwa shampoo nzuri (isiyo na viambata sumu)
🧚‍♀️Usitumie  shampoo zenye viambata sumu kama vile sulphate kwa sababu ni kemikali ambayo si rafiki kwa nywele hasa natura;  unaponunua shampoo hakikisha unasoma ingredients kwa umakini na kuhakikisha ni sulphate free shampoo
🧚‍♀️Chana  nywele zako vizuri ikiwezekana tumia mikono kwanza wakati wa kuchambua kisha zichane maana vipilipili vyetu (nywele nyingi za kiafrica) zina  tabia ya kujifunga sana
🧚‍♀️Fanya  steaming (deep conditioner) mara kwa mara na ikiwezekana hata kila wiki.
🧚‍♀️Tumia  satin cap wakati wa kulala; unaweza kvaa kofia ya satini au mto wako uvishe foronya ya satini.
🧚‍♀️Suka  misuko kinga ili kulinda nywele zako kila wakati na hufanya nywele kukua, na kuzuia kukatia /misuko kinga yaani PROTECTIVE  style
🧚‍♀️Zipe  nywele zako unyevu; Maji maji  ni rafiki wa nywele hasa nywele natural,ndio maana unatakiwa uwe na spray bottle (kinyunyuzi) kiungo kikubwa katika kuzipa nywele unyevu ni maji huwezi kuwa naturista kama huna spray bottle.
🧚‍♀️Trim  nywele zako yaani ondoa  nywele zisizo na afya na zenye dawa,mpaka utakapobaki na nywele natural tu. Pia kwa wenye natural hair   trim zile nywele za  juu zisizo na afya mara kwa mara
🧚‍♀️Usitumie taulo kufuta nywele zako bali tumia  t-shirt hasa ya cotton kufuta nywele zako.
NB: Ni lazima uwe na tshirt maana t-shirt  inabaki na nywele na pia huvuta  nywele kitu ambacho kinachangia sana katika  kukatika kwa nywele.
🧚‍♀️Chana nywele  zako kwa mafungu pindi unapoosha
NB: kufanya hivyo kunasaidia nywele zako kutakata maana unaosha kidogo kidogo tofauti ukiosha kwa jumla unakata mafungu manne au zaidi kulingana na uwingi wa nywele zako.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad