NJIA 10 ZA KUFANYA NYWELE ZIWE ZA KUVUTIA NA ZENYE AFYA

kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa yanayowekwa  kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika,  kukosa afya pamoja na  mvuto. leo nimekuletea vidokezo vichache vya jinsi ya kutunza nywele zako kiusahihi zaidi.
🧚🏻‍♂️Kata ncha za nywele zako
kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. Seli zinapokufa huzuia  nywele zinazozaliwa  kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. Japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi lakini  ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.

🧚🏻‍♂️Osha  nywele zako angalau mara moja kwa wiki
Kuosha  nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya na safi; hata  kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuziosha  nywele zako.

🧚🏻‍♂️Tumia  shampoo inayoendana na nywele zako
Tumia  shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu, nzito nk.. Zipo  aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo, hivyo  basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.

🧚🏻‍♂️Zipe  nywele zako nafasi
Nywele  nazo huitaji nafasi,kuchana nywele kila siku,  kuzipaka nywele jelly kila siku, kuzichana mitindo tofauti, kuziwekea gundi na mafuta tofauti tofauti huzifanya nywele zako zichoke na kukosa afya, hivyo  unatakiwa mara moja moja unazipa nywele zako nafasi ya kupumzika na kupumua  kwa kusuka mtindo ya kawaida au rasta za mabutu. ​

🧚🏻‍♂️Usichane  nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.
Jaribu  kuzichana nywele kwa chanuo kubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibu ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.

🧚🏻‍♂️Zilinde  nywele zako unapokuwa unaogelea
Unapokua  unaogelea baharini au kwenye bwawa la kuogelea, jaribu kuzifunika nywele zako au zipake mafuta ya kuzuia  zisiharibike na maji, na unapotoka kuogelea zisafishe nywele zako kwa maji safi na uzikaushe.

🧚🏻‍♂️Kula  vyakula venye protein na matunda kwa wingi
kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimarisha  afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.

🧚🏻‍♂️Zifunge  nywele zako kabla ya kulala
Unapotaka  kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifunga  vizuri na kuzibana. Kulala huku  ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika

🧚🏻‍♂️Tumia  mafuta asili
Badala  ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. Tumia  mafuta kama ya mnyonyo au  nazi au parachichi kupaka nywele zako.

🧚🏻‍♂️Zilimde  nywele zako na jua
Wakati  utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. pia unaweza kuzipaka sunscreen.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad