UMUHIMU WA MAJANI YA MPERA (GUAVA LEAVES) KWENYE NYWELE

Majani ya mpera ni mazuri sana kwa ukuaji wa nywele hasa asilia (Natural hair) kwa sababu;
-Yana Vitamin B (Biotin ambayo ni nzuri sana katika ukuaji wa nywele) ya kutosha ambayo ipo pia kwenye brands kubwa za products za nywele; hapa wanainfuse biotin ili kuongeza effciency na effectiveness ya product. Biotin pia inapatikana kama supplement (zinamezwa) hii yote ni kufanya nywele kukua vizuri kwa kupata nutrients za kutosha.
-Yana vitamin C; hii inasaidia sana kwa sababu ni anti-oxidant na pia ni anti inflammatory (kuzuia kuwasha, kuvimba au maumivu in case umeungua na dawa na vinginevyo)

Majani ya mpera yanaweza kutumika kama steaming au leave in conditioner. Leo tutaongelea zaidi kama Leave in Conditioner (kuzipa nywele unyevu tu na ukitumia hauoshi tena).

FAIDA ZA MAJANI YA MPERA KAMA LEAVE IN CONDITIONER
-Yanasaidia kuilinda ngozi dhidi ya maradhi kama mba, fungus na infections nyingine.
-yanasaidia kurudisha rangi nzuri ya nywele (nyeusi) kama nywele ni nyekundu au zina mvi.
-Inasaidia nywele kukua vizuri na kuwa imara
-Inafanya nywele kuwa na afya.
-yanasaidia kuzuia nywele kukatika
-Pia ni gharama nafuu, ya asili kabisa (hayana chemicals) na ni rahisi sana kuyapata ukilinganisha na leave in conditioners za kununua.

JINSI YA KUANDAA
-Chukua majani malaini kama 10 hadi 20
-Weka kwenye sufuria na ongeza maji kidogo (lita moja)
-Funika na acha yachemke vizuri hadi yabadilike rangi kuwa kama chai ya rangi
-Baada ya dakika 5 ipua na uache yapoe.
-Baada ya kupoa weka kwenye spray bottle yako; utakua unazipa unyevu nywele kwa kutumia maji hayo halafu juu unapaka mafuta ukifuata LOC Method (Pitia posts zilizopita).

Pia unaweza kuchanganya na mafuta (Black castor oil, jojoba oil, coconut oil au olive oil; any of your choice) ili yaingie vizuri kwenye nywele.

NB: Maji hayo yanaweza kaa hadi wiki ukiweka kwenye fridge, otherwise ni siku mbili tu (maximum).

Pia ili kuona matokeo mazuri ya product yoyote ya nywele au ngozi ni lazima utumie kwa muda mrefu na kwa mpangilio unaotakiwa (consistency).

CONSISTENCY IS THE KEY TO GOOD HAIR.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad