JINSI YA KUTUMIA MAJANI YA CHAI KWENYE NYWELE

Majani ya chai yoyote yale yawe ni yale ya kawaida, green tea au rosemary yana umuhimu sana katika ukuaji wa nywele. Wengi hutumia maji yake katika kusuuzia nywele (Wengi huita Rinse out tea); hapa unaweza tumia vitu mbali mbali tutazidi kuviangalia kwenye posts zinazofuta.

FAIDA ZA MAJANI YA CHAI KWENYE NYWELE
-Yanajaza nywele
-Yanang’arisha nywele
-Yanarudisha rangi ya asili ya nywele zako na kuzipendezesha zaidi
-Yanazuia nywele kukatika
-Yanarefusha nywele kama inavotakiwa

NB: Kuna njia nyingi za kutumia maji ya majani ya chai kwenye nywele
1. Unaweza kuchanganya kwenye steaming yako
2. Unaweza kusuuzia nywele zako baada ya kuosha

NJIA YA KWANZA
-Chukua vijiko vitatu vya majani ya chai weka kwenye sufuria safi
-Baada ya hapo ongeza maji nusu lita
-Acha yachemle kwa dakika 5 hadi 10 kisha yaache yapoe kabisa
-Baada ya hapo chuja upate maji ya majani ya chai bila makapi
-Baada ya kuosha nywele na shampoo na kusuuza na maji ya kawaida zimwagie nywele zako maji hayo uliyoandaa (ukimaliza hapo usioshe tena nywele)
-Unaweza endelea kupaka steaming yako uliyoiandaa

NJIA YA PILI
Mahitaji
-Vijiko vitatu (3) vya maji ya chai
-Tui la nazi
-Mafuta ya nywele (Castor oil/Coconut oil)

JINSI YA KUFANYA
-Changanya vyote kwenye bakuli moja
-Paka kwenye nywele zako vizuri
-Vaa kofia ya plastic au kaa kwenye steamer kwa dk 30 hadi 45.
-Osha nywele zako vizuri na maji ya kawaida halafu unaweza suuza tena na maji ya chai uliyokwisha andaa hapo awali.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad