19. NYANYA NA FAIDA ZAKE

Mbali na kuwa kiungo muhimu katika upishi, nyanya inaweza kutumika kama njia au dawa ya kupambana na mafuta mengi katika ngozi ambayo kwa namna moja au nyingine husababisha kuharibika kwa ngozi au kusababisha uwepo wa chunusi.

Tatizo la mafuta usoni limewakosesha raha watu wengi na wamekuwa wakitafuta dawa ambazo huenda zikaongeza tatizo.
Hii ni kwa sababu nyingi ya dawa hizi zina kemikali hatari kwa ngozi ya uso.
Ili kujiepusha na tatizo hilo au athari hizo, unaweza kutumia nyanya kama njia salama ya kuondoa mafuta usoni.

Virutubisho vinavyopatikana kwenye nyanya ni Vitamin A,C na K na madini kama potassium na madini ya chuma, shaba, na protini n.k vinasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na mafuta ya ziada ambayo hayahitajiki mwilini.

JINSI YA KUANDAA
🍅Kata  nyanya vipande viwili
🍅Safisha uso wako kwa maji ya vuguvugu kisha kausha kwa taulo au kitambaa safi.
🍅Baada ya kuhakikisha kitambaa kimekua kikavu,chukua kipande cha nyanya na uanze kupaka kwa utaratibu katika uso na uhakikishe maji yake yanabaki usoni.
🍅Acha maji hayo yakae usoni kwa dakika kama 20 kisha safisha uso tena kwa maji ya uvuguvugu.
🍅Unaweza pia kusaga nyanya na kupata juice yake ikiwa nzitoambayo itahitaji kuchanganya na maji kidogo pamoja na juice ya limao na kupata mchanganyiko ambao utasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa mafuta katika ngozi yako.
🍅Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi angalau kila siku kabla ya kulala au baada ya cku mbili na kwa mwezi mmoja matokeo yataonekana katika ngozi yako na kuifanya ivutie na kuwa na mng’ao.

Watu wengi wanadhani kutumia vitu vya asili ni urembo wenye mchakato mrefu na mgumu lakini kama unaipenda ngozi yako naamini hutaona ugumu wa kuitunza kwa vipodozi vya asili.


JINSI YA KULAINISHA USO KWA NYANYA NA ASALI
🍅Chukua nyanya moja kubwa iliyoiva kisha imenye na kuisaga kisha ipake usoni
🍅Ukimaliza chukua asali mbichi na uchanganye usoni na nyanya
🍅Baada ya hapo acha kwa robo saa hadi ikauke kisha nenda kanawe
🍅Kausha uso vizuri na taulo safi na rudia hivyo mara mbili kwa wiki na utapata matokeo mazuri kwa ngozi ya uso ,na njia hii inawafaa zaidi wenye chunusi ,kwani huwasaidia katika matatizo kama hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad