18. UMUHIMU/FAIDA ZA KULALA NA KOFIA YA SATINI

KOFIA ZA SATINI/SATIN CAPS

 
Kofia hizi zinaonekana kama ni kitu kidogo sana au ni extra sana lakini  katika kutunza nywele zako (iwe za dawa au za asilia) ni kitu muhimu snaa ambacho ni ngumu sana kukipotezea. Kofia za satini (za kulalia) zina faida nyingi sana; ikiwemo zifuatazo;

🌸Kofia hizi ni special au nzuri kwa sababu zinalinda vizuri unyevu wa nywele.
-Material ya satini ni laini hivyo unyevu wa nywele ni ngumu kupotea kirahisi kama ambavyo mtu atakala na kitambaa/mto/ foronya au kofia ya material nyingine kama vile pamba (cotton) ambapo materials hizi sio rafiki kwa nywele maana hunyonya au kufyonza mafuta na unyevu wote kutoka kwenye nywele.

🌸Kuzuia nywele kukatika
-Satin hairuhusu upotevu wa mafuta kwenye nywele haraka, nywele zetu zibaki laini hivo hazitokatika kama nywele kavu.

🌸Kutunza style ya nywele kwa muda mrefu.
-Style ya nywele haitovurugika haraka endapo utalala umevaa kofia ya satin. Utaamka asubuh ikiwa bado umependeza😍😍

🌸Kuzuia nywele kujisokota/kujifunga
-Nywele zetu za kiafrika zina curls au mawimbi sana. Zikiwa hazijasukwa na ukalala bila kofia utasababisha nywele kujifunga sana, na hili linaweza sababisha nywele kukatika.

🌸Hupendezesha na kukupa muonekano mzuri😜😜

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad