21. MADHARA YA MOTO KWENYE NYWELE NA JINSI YA KUUEPUKA

🔥Kwa hair lovers wote hakuna kitu kinachoua nywele (natural au relaxed) kama matumiz ya moto unaotokana na dryer, blow dryer, pasi, detangler ya umeme n.k

🔥Wengi wanaamini njia pekee ya kukausha au kunyoosha nywele ni kutumia moto lakin hayo ni makosa makubwa sana katika utunzaji sahihi wa nywele.

MADHARA YA MOTO KWENYE NYWELE
⚡️Inakausha unyevu wote ulioko kwenye nywele na kupelekea kuwa  kavu na kukatika.
⚡️Inaharibu hair structure (mpangilio wa nywele) na kuwa dhaifu.
⚡️Inaharibu protein bonds za nywele na kua dhaifu sana.
⚡️Inaunguza hair layer nakuifanya dhaifu
⚡️Inabadili rangi ya nywele yako ilivyokua nyeusi na kua ya brown/nyekundu

NINI KIFANYIKE
🌿Baada ya kuosha nywele kausha na Tshirt ya cotton au micro fiber towel.
🌿Baada ya hapo paka nywele zako leave in conditioner (water based product)
🌿Baada ya hapo paka mafuta ya maji halafu malizia na cream/shea butter
🌿Halaf unaweza kusuka nywele ya uzi ,twist au hata ukasuka hakuna shida yoyote

KWA WALE AMBAO NYWELE ZISHAHARIBIKA NA MOTO
🔥Wale ambao mlikua mnatumia moto sana inamaana kwasasa nywele zenu zina heat damage na ndio maana nywele zenu hazijai wala kuota vizur tena kwakua zimeharibiwa na moto

FANYA YAFUATAYO
Yafuatayo yatakusaidia kurudisha nywele zako katika hali nzuri

🌿Andaa hair routine nzuri uwe unafanya steaming(deep conditioner) mara kwa mara kama ya protein mara moja kwa mwez na nyingne water based products/steaming za kawaida
🌿Acha kabisa kutumia moto tena iliusiharibu nywele zako tena.
🌿Tumia natural products kwenye nywele yako kama parachichi, ndizi, asali, majani ya mpera ,mlonge, n.k zitasaidia kurudisha nywele yako kwa hali ya kawaida kwakua hizi zinadirect nutrients kwenye nywele yako.
🌿Kurudisha nywele kua katika hali yake inategema kwakua kila nywele inategemea inaharibika kwa kiwango gani.
Kwahiyo ushauri wangu usitumie moto tena kausha nywele yako kawaida (air drying)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad