22. FAHAMU ZAIDI KUHUSU MAFUTA YA MNYONYO (CASTOR OIL)

🌿Katika miaka ya karibuni bidhaa zinazohusiana na ngozi na nywele zenye "castor oil" zimekua na umaarufu mkubwa katika matumizi ya kila siku duniani.
🌿Castor oil ni mafuta ya mnyonyo ambayo hutokana na mbegu za mmea uitwao mbarika au mbono
🌿Nyonyo hulimwa ili kupata mbegu zake na asili yake ni Afrika Mashariki na Afrika kusini, ila hustawi pande zote za dunia zilizo katika tropic na jirani ya tropic
🌿kati ya asilimia 45 na 60 ya mafuta yapatikanayo kwenye nyonyo huwa na madini mengi aina ya ricinolein..
🌿Nyonyo ni miongoni mwa vyanzo vya sumu kali iitwayo ricin. Hivyo basi ni vyema kuepuka kula nyonyo zilizosindikwa na hata kama zimesindikwa ni sharti ziwe zina alama inayoonesha kuwa yafaa kwa matumizi ya kula.
😋🌿Kila kitu kinachopatikana kwenye mmea wa mnyonyo kina faida za kiafya kwenye mwili wa binadamu.

MAJANI YA MNYONYO
⚡️Tiba ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB)
⚡️Huleta nafuu kwa mguu ulioteguka
⚡️Hutumika kutibu uvimbe kwa wanyama
⚡️kikonyo ni dawa ya kwikwi

MZIZI
⚡️Hutumiwa kama dawa ya mafindo findo, uvimbe, kuungua, macho ya njano,kuumwa koo na magonjwa ya kuambukiza ya kisonono na kaswende

MBEGU/PUNJE
Hutumika kutengenezea mafuta ambayo;
⚡️Hutibu maumivu yaliyosababishwa na kuungua
⚡️Kulainisha mashine na mitambo viwandani.
⚡️Mafuta ya mnyonyo huwa na Ricinoleic acid, oleic acid, linoleic acid n.k ambazo hutibu ugonjwa wa jongo (rheumatism) unaowakumba watu wengi wanaoishi maeneo ya miinuko na baridi, ⚡️hutibu ugonjwa wa mifupa ujulikanao kitaalam kama Arthritis na gauti.
⚡️Yanaweza kutumika kama njia ya kupanga uzazi
⚡️Kurekebisha hedhi na kupunguza maumivu
⚡️Kutibu vidonda vilivyosababishwa na bacteria na ukungu (fungus)
⚡️Hutibu ngozi iliyobabuka kwa moto au jua kali sana
⚡️Hupunguza kasi ya kuzeeka
⚡️Hupunguza chunusi na kufanya ngozi kuwa na unyevu wa kutosha
⚡️Husaidia kuondoa makovu madogo dogo
⚡️Huimarisha ukuaji wa nywele
⚡️Hutibu maambukizi yaliyo kwenye ngozi ya kichwa
⚡️Huzuia michirizi
⚡️Huzuia maoteo ya nywele yasikatike
⚡️Hupunguza vidoti doti kwenye ngozi, hutumika kulainisha choo
⚡️Hupunguza maumivu ya viungo na pia huongeza kinga mwilini
⚡️Mafuta ya mnyonyo yanaweza kumfaa mtu mwenye VVU kwan mafuta yake ni sumu ya kuua vimelea vya magonjwa
⚡️Hutumika kutengenezea sabuni, karatasi angavu, wino wa printer na vanish,hutumika kwa ajili ya kuzalisha dawa mbalimbali za matibabu, mmea huu pia huweza kutoa mbolea

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad