7. KWA WALE WANAOISHI SEHEMU ZENYE BARIDI.

I hope these tips zitawasaidia, kumbuka tuna nywele na genes tofauti, wengine wakiwa kwenye baridi nywele zinakua zaidi ila wengine ndio nywele haikui
TIPS
🍃Usioshe nywele mara kwa mara, unaweza kuwa na utaratibu wa kuosha nywele mara 2 au 3 tu kwa mwezi, na hapa utatumia shampoo.
-Nasema hivi kwa kuwa kuna wengine bado wanatumia maji ya chumvi au shampoo zenye sulfate, hii inaondoa mafuta yote na unyevu wote nywele inakua kavu mno, hii ni tofauti na kuspray mara kwa mara.

🍃Tumia maji ya uvuguvugu kuspray nywele zako au hata kama unatumia majani ya mpera warm the water.
-Tunafanya hivi kwa sababu hair pores zikipata ubaridi zinajifunga so kwa hali ya kawaida zinahitaji joto ili zijifungue na ww keep in mind kua joto ni muhimu kwa nywele na baridi ikipita pores zinajifunga and you are good to go.

-Usipake mafuta yaliyoganda au ya mgando (hapa najua kuna wengine ata mafuta ya nazi yanaganda) hayasaidii muhimu mafuta yaingie kwenye ngozi, sasa ukitaka kupaka mafuta chemsha maji weka kwenye bakuli halafu weka kopo la mafuta yako au mafuta kdg ambayo unataka kutumia then ndio upake.

-Steaming ni muhimu kwa kuwa ni njia pekee ambayo nywele zako zinapata nutrients; na hapa kwenye steaming joto linahitajika ili pores zako ziweze kufunguka.
-Na hapa hakuna njia nyingine zaidi ya kwenda saloon uingie kwenye steamer au kama una blow dryer nyumbani bas pitisha kwa juu ili joto liingie na baada ya hapo utaosha.
Kumbuka kuanza na maji ya uvuguvugu.

🍃Unahitaji good sealing oil.
Kazi ya sealing oil ni kuzuia nywele au ngozi isipate ukavu kwa haraka, ile moisturizer uliyospray baadae juu isikauke kwa haraka.
-When your hair is well sealed hata upepo ukipita utaanza kuaffect mafuta kwanza na sio nywele au ngozi/scalp direct.

Nazi/coconut oil sio sealant/sealing oil..je ww unatumia nini kuseal in moisture?

ITAENDELEA....

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad