35. JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA NAZI

Ni kwa muda sasa nmekua nikishauri watu watumie mafuta ya asili (ambayo hayana kemikali) kwenye nywele na ngozi zai lakini kwa wengi imekua challenge kuyapata mafuta mazuri kwa muda; na wengi wamekua na maswali mengi sana kuhusu jinsi ya kutengeneza mafuta ya nazi nyumbani (baada ya kuwashauri kutumia mafuta ambayo wametengeneza wenyewe) ambayo ni safe zaidi kuliko ya kununua. Leo ntaelekeza njia tatu tofauti utakazoweza kutumia ili kupata mafuta ya nazi.


NJIA YA KWANZA
🧚🏻‍♂️Chukua nazi iliyokomaa vizuri
🧚🏻‍♂️Iache mpaka iharibike
🧚🏻‍♂️Baada ya hapo toa nazi na uweke kwenye blender, food processor au kikunio  ili iweze kulainika
vizuri
🧚🏻‍♂️Ongeza  maji ya vuguvugu na kamua  tui
🧚🏻‍♂️Chemsha  tui na mchai chai pamoja mpaka uone mafuta yanabakia,
🧚🏻‍♂️Ondoa  majanu ya mchai chai  na kutoa mafuta yako na kuyaweka kwenye chombo chako ili utumie.
NB:  Njia hii inakufanya uweze kupata mafuta mengi zaidi na pia mchai chai una manufaa  sana katika kufanya mwili na ngozi (hasa ya kichwa)  kurelax  sasa ukichanganya wakati wa kuchemsha utaweza kupata virutubisho vyingi zaidi kwenye mafuta; ambavyo vitakua na faida kwenye nywele pamoja na ngozi.

Pia mara  nyingine mafuta ya nazi huwa na harufu, usiwe na shaka hapa pia nitakupa njia ya kuondoa harufu iyo na kubaki na harufu iliyopoa.

JINSI YA KUONDOA HARUFU KWENYE MAFUTA YA NAZI
🍃Chukua  sufuria kubwa weka maji na kuyaweka kwenye moto. (medi-High temperature yaani moto wa kawaida usiwe mkali sanaa).
🍃Chukua  sufuria ndogo weka mafuta yako ya nazi.
🍃Chukua mchai mchai (green tea. Changanya kwenye mafuta yako.).
🍃Weka sufuria  yenye mchanganyiko wa mafuta na mchai chai  juu ya safuria yenye maji na kupika kwa muda wa dakika kama 30 hivi.
🍃Ondoa majani na weka mafuta yako kwenye chombo cha kutumia.
🍃Mafuta yako yatakua tayari kutumia.

ITAENDELEA NIKIELEZEA NJIA YA PILI NA YA TATU

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad