34. NAMNA AMBAVYO NYWELE ZAKO ZINAWEZA KUHARIBIKA

Leo tuongelee jinsi gani nywele zako zinaweza kuharibika na namna ambavyo unaweza kuepuka tatizo hilo.
Kuharibika kwa nywele kunasababishwa na vitu vingi sana na kuna aina tofauti tofauti za kuharibika kwa nywele. Hii hutokea kwa nywele zote ziwe zina dawa na ambazo hazina dawa na hii inadhihirishwa na kuwa na nywele ambazo hazina mvuto. Unaweza kuwa na nywele ambazo hazieleweki kama zina dawa au hazina dawa, nywele zinakua mbaya mpaka mwenyewe haupo proud nazo.

AINA ZA KUHARIBIKA KWA NYWELE
🧚🏻‍♂️Heat damage (Matumizi ya moto): 
Hii inasababishwa na kutumia moto wa aina yoyote ile kukausha nywele iwe ni dryer, pasi nk. Moto huu huwa ni mkali sana na unakausha unyevu wote kwenye nywele ndani na nje na pia hufanya nywele kuwa dhaifu na nyepesi mno na kupoteza mvuto. Hivyo basi usitumie moto wa aina yoyote ile katika kukausha nywele zako.

🧚🏻‍♂️Chemical damage (Uharibifu unaotokana na viambata sumu):
Hii inasababishwa na kutumia products zenye viambata sumu kama vile shampoo, conditioner, hair treatments zenye sulphates, parabens, harmful alcohols, mineral oils, petroleum etc. hizi zinaharibu sana nywele and its important kusoma labels zote za vitu unavyotumia kabla ya kutumia kwenye nywele zako. Zipende nywele zako.

🧚🏻‍♂️Hair dryness/kuwa na nywele kavu
Hii inasababishwa na vitu vingi lakini kitu cha muhimu kuliko vyote ni kutokuzipa nywele unyevu. Watu wengi wamekua wakiruka step ya kupaka leave in conditioner na wanakimbilia kupaka mafuta (hapa nywele zitaendelea kuwa kavu tu hata ufanyeje maana una seal in dryness na sio moisture) so ni muhimu kuanza na kupaka leave in conditioner ndio ufate mafuta then Cream (shea butter) katika LOC Mthod ili nywele ziwe na unyevu na zisikatike kirahisi. Pia inatakiwa kujenga utamaduni wa kuzispray maji yaliyochanganywa na leave in conditioner at least mara tatu kwa wiki.

🧚🏻‍♂️Mitindo au misuko hatarishi/ kusuka mara nyingi/ kutozipumzisha nywele
Hapa ukiwa na tabia ya kufanya lolote kati ya hayo matatu, una hatari ya kuwa na nywele dhaifu sana, maana kuna watu anafumua nywele leo na kusuka siku hiyo hiyo bila kuzifanyia nywele treatment yote (sio steaming wala protein treatment) nywele zinakosa muda wa kupumua hivyo zinakua dhaifu.
-Pia mtu anaweza kusuka nywele kama Afro kinky na anakaa nazo zaidi ata ya miez mi3 so its obvious nywele lazima zichoke na utakuta wakati wa kufunua zinakatika tu maana ndani ya hiyo miez mitatu utakuta hakuna cha unyevu wala mafuta yeye ni kubana tu tena once per month, hapo lazima nywele ziharibike.
-Pia kuna watu wanasuka misuko hatarishi unakuta edges (vimalaika) vimevutwa hadi vinakatika na kuzikuza tena inakua shida.
-Pia umakini unatakiwa maana kuna wasusi wanatumia majivu kushikia nywele za mbele katika baadhi ya misuko, huo ni uchafu na nywele zitaendelea kukatika every now and then.
-Inatakiwa uzipe nywele muda wa kurelax na gap kati ya msuko na msuko, sometimes unaweza kubana style yako nzuri for a week just kuzipa nywele relaxation period.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad