37. JINSI YA KUONDOA MBA KWA KUTUMIA MUARUBAINI (NEEM LEAVES)

Tumekua tukiongelea sana suala la kuondoa mba lakini bado kuna wengine wanapata changamoto ya kushindwa kuondoa mba kwenye nywele zao. Mba unatesa sana, unakua huna raha, kila muda unajikuna na wengine huishia kunyoa nywele zao kisa mba. Leo tuangalie njia nyingine ambayo unaweza kufanya kuondoa mba kabisa ambayo pia ni tiba nzuri kwa nywele, mapunye, mba, vidonda kichwani nk.

MAHITAJI
🧚🏻‍♂️Majani ya muarubaini
🧚🏻‍♂️Mafuta ya nazi/Mafuta ya mnyonyo
🧚🏻‍♂️Shower cap

JINSI YA KUFANYA
🧚🏻‍♂️Chukua majani yako ya mwarobaini yaoshe vizuri
🧚🏻‍♂️Chemsha majani hayo ndani ya dk 10 hadi 15
🧚🏻‍♂️Chuja mchemsho huo kisha upate maji ya miarobaini
🧚🏻‍♂️ Ongeza vijiko viwili vya mafuta (utakayochagua wewe)
🧚🏻‍♂️Weka mchanganyiko huo ukae masaa 12 ukiwa umetulia ili kupunguza nguvu
🧚🏻‍♂️Baadae osha kichwani huku ikisugua ngozi ya kichwa  na mchanganyiko huo
🧚🏻‍♂️Ukimaliza vaa shower cap na kaa nayo kwa muda wa dk 30
🧚🏻‍♂️Kisha osha nywele zako na maji safi

NB: Majani ya muarobaini yana faida nyingi sana kwenye nywele ikiwa ni pamoja na;
🍃Kutoa na kuzuia mba
🍃Huzuia nywele kukatika
🍃Kutibu mapunye, vidonda na miwasho
🍃Kufanya ngozi ya kichwa ilainike na kurelax.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad