38. KWA NINI NYWELE ZAKO HAZIKUI

Hili ni swali ambalo watu wengi wamekua wanauliza, mbona nywele zangu hazikui, imekua miaka kadhaa toka nianze kufuga nywele lakini ziko pale pale, haziongezeki wala kukua. Nataka tu nikukumbushe leo nywele hazijawahi kuacha kukua na wala hazitaacha kukua, zitaendelea kukua mpaka siku unayofariki (kuondoka duniani). Kama nywele zako zimekua na ujazo na kimo hivho hicho kwa muda mrefu jua kua nywele zako hazijaacha kukua ila zinakatika (kiwango kinachokua ni sawa na kinachokatika au kinachotoka/so work done=zero). Kwa hiyo swali unalotakiwa kujiuliza ni kwa nini nywele zako zinakatika?.
Hizi ni baadhi ya sababu kwa nywele kukatika

🧚🏻‍♂️Namna ya kustyle na kubana nywele kwa kutumia gels mbalimbali na kukaa nazo muda mrefu
🧚🏻‍♂️Detangling isiyo sahihi (kutumia nguvu na kufanya haraka haraka)
🧚🏻‍♂️Viambata sumu (harmful chemicals)
🧚🏻‍♂️Misuko hatarishi inayokaza sana nywele
🧚🏻‍♂️Overstyling (kubana sana nywele kwa muda mrefu)
🧚🏻‍♂️Kukosa umakini na nywele zako
🧚🏻‍♂️Kutotumia vifaa sahihi
🧚🏻‍♂️Kukosa unyevu na kutreat nywele zako zikiwa kavu
🧚🏻‍♂️Njia za kutunza nywele zisizo sahihi
🧚🏻‍♂️Kudetangle nywele kavu
🧚🏻‍♂️Kutokukata ncha
🧚🏻‍♂️Kutopata mlo kamili na kutokunywa maji ya kutosha
🧚🏻‍♂️Kuzipa nywele zako protein nyingi (Too much protein treatment)
🧚🏻‍♂️Kukosa kabisa protein

MOST IMPORTANT: Zipende nywele zako nazo zitakupenda na hayo yote👆🏿👆🏿 unaweza kuyafanya endapo tu utazipenda nywele zako

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad