UTAJUAJE KAMA NYWELE ZAKO ZINA AFYA (HEALTHY HAIR)

Unaweza kuwa na nywele ambazo unaweza kukaa nazo lakini hujui kama ni nywele zenye afya au lah; Jaribu kuzichunguza vizuri nywele zako na kama zina sifa zifuatazo basi ni nywele zenye afya

🧚🏻‍♂️Hazikatiki kabisa au zinakatika kidogo sana

🧚🏻‍♂️Zinang’aa naturally
Hapa nywele zinakua zinang’aa vizuri na kuvutia hata bila kutumia sprays.

🧚🏻‍♂️Zinakaa na kupokea unyevu kirahisi

🧚🏻‍♂️Zinakua laini na haziuki wakati wa kuchana
Hapa hata kwenye kudetangle inakua ni rahisi sana unaona kabisa vidole vinapita kirahisi zaidi na hata ukizipa  unyevu inakua ni rahisi sana kuzichana

🧚🏻‍♂️Zinakua na nguvu (sio nyepesi sana) na kuwa nzito
Hapa nywele zinakua na nguvu na hata pale unapochana unaona kabisa kukatika ni ngumu sana labda utumie nguvu zaidi au ukosee uchanaji wake.

🧚🏻‍♂️Uwezo wa kuvutika kirahisi
Hapa hata kama nywele zako zimeshrink (ambayo ninsifa pia ya nywele zenye afya) lakini zinakua na uwezo wa kuvutika maana yake nywele sio ngumu ila ni nzito.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad