JINSI YA KUKUZA NYWELE KWA HARAKA ZAIDI

Leo tuangalie treatment au steaming unayoweza kuifanya mara kwa mara ili upate nywele ndefu na zenye afya baada ya muda mfupi sana (Baada ya mwezi unaanza kuona mabadiliko). Hii treatment inatumika kwa watu wenye nywele za aina yoyote.

Mahitaji
🧚🏻‍♂️Yai moja la kienyeji
🧚🏻‍♂️Hinna ya unga

JINSI YA KUANDAA
🧚🏻‍♂️Tengeneza mchanganyiko wa yai (lote) na hinna kiasi ili upate mchanganyiko mzito kidogo (paste).
🧚🏻‍♂️Paka katika mizizi ya nywele
🧚🏻‍♂️Ukimaliza kupaka vaa shower cap
🧚🏻‍♂️Unaweza funga na lemba juu ya shower cap ili zipate joto zaidi
🧚🏻‍♂️Kaa navyo kwa muda wa masaa mawili
🧚🏻‍♂️Baada ya hapo osha kwa maji ya kawaidia na shampoo
NB: Tumia maji mengi ili kuondoa harufu ya mayai, pia yawe ya baridi (yasiwe ya moto wala vuguvugu-utapata harufu ya mayai ya kuchemsha)
🧚🏻‍♂️Kausha nywele zako kwa tshirt au kitambaa cha cotton
🧚🏻‍♂️Fanya hii kila wiki utapata matokeo ya haraka zaidi

Mambo ya kuzingatia
🧚🏻‍♂️Nywele hazichanwi zikiwa na maji (zikiwa mbichi); Hii husababisha kung'oka kwa nywele na kusababisha upungufu wa nywele (nywele kuwa chache).
🧚🏻‍♂️Nywele zikishakauka, paka  mafuta ya nazi, au your favourate muhimu upake katika mizizi ya kichwa na upende zaidi kutumia mafuta ya kimiminika au ya maji
🧚🏻‍♂️Wakati unapaka mafuta kichwani kichwa kiinamishe chini, kiangalie chini ndio upake mafuta kichwa chako husaidia msukumo wa damu kufikia katika kichwa vizuri, kupata stimulation tumia ncha za vidole kufanya massage kichwani taratibu kwa mda wa dakika tano, ukimaliza anza kuzichana taratibuu mpaka zilainike na uzibane.
🧚🏻‍♂️Jaribu kwa siku uchane nywele mara mbili asubuhi na jioni (kama hujasuka), na nywele muda wote ziwe zenye mafuta. 
🧚🏻‍♂️Jizoeshe m kufanyia massage kichwa chako kila wakati unaopaka mafuta kichwani.

KUMBUKA: Uhai wa nywele ni mafuta na maji kama  ilivyo uhai wa binadamu utakuepo iwapo kuna maji na chakula
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad