MAFUTA MAZURI YA NYWELE AINA ZOTE

Tulishaangalia aina mbili za mafuta mazuri ya nywele aina zote, leo tumalizie aina ya tatu ili kila mmoja aweze kuchagua mafuta yake anayotaka ayatumie na yatakayomletea matokeo chanya.

AINA YA TATU: MAFUTA YA NAZI (COCONUT OIL)


Haya ni mafuta ambayo yanajulikana sana na watu wengi kuipelekea kupewa jina la “Mafuta mama”. Mafuta haya yapo ya aina nyingi sana kutegemea na njia anayotumia mtu kuyatengeneza, pia yapo fake na original (kuwa makini wakati wa kuchagua). Siku zote tumia ambayo yameandikwa “VIRGIN COCONUT OIL” au “MAFUTA MWALI” haya ndio huwa pure means hayajachakachukiwa.
Mafuta ya nazi yana matumizi mbalimbali tofauti na urembo wa ngozi na nywele. Umaridadi wake unatokana na uwepo wa asidi mafuta muhimu sana ya “Lauric” ambayo ina uwezo wa kupambana na bacteria, fangasi, sumu, vijidudu nyemelezi na maambukizi. Mafuta haya yanatumika kupikia pia.

Faida  za mafuta ya nazi  (urembo)
🧚🏻‍♂️Hukuza na kurefusha nywele kwa muda mfupi
🧚🏻‍♂️Huondoa mba na kulainisha nywele
🧚🏻‍♂️Hutibu matatizo yote ya magonjwa ya ngozi kichwani
🧚🏻‍♂️Hulainisha ngozi
🧚🏻‍♂️Husaidia kuzipa nywele unyevu unyevu

Faida za mafuta ya nazi (mengineyo)
🧚🏻‍♂️Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
🧚🏻‍♂️Huzuia uwezekana wa kupata kansa
🧚🏻‍♂️Yanaongeza kinga ya mwili maradufu
🧚🏻‍♂️Yanaongeza nguvu ya ubongo
🧚🏻‍♂️Dawa nzuri ya kutibu matatizo ya mifupa
🧚🏻‍♂️Husaidia kushusha uzito (kupunguza uzito)
🧚🏻‍♂️Husaidia kuondoa msongo wa mawazo (stress)
🧚🏻‍♂️Huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
🧚🏻‍♂️Hutibu matatizo ya kongosho na kibofu cha mkojo
🧚🏻‍♂️Yanatibu na kuimarisha mfumo wa misuli ya mwili
🧚🏻‍♂️Huzuia meno kuoza na maradhi ya fizi
🧚🏻‍♂️Huongeza ufanisi wa ini na figo
🧚🏻‍♂️Yanaondoa mawe kwenye figo na kibofu cha mkojo
🧚🏻‍♂️Yanaondoa baridi yabisi
🧚🏻‍♂️Yanatibu kisukari aina ya kwanza
🧚🏻‍♂️Yanatibu maambukizi ya fangasi
🧚🏻‍♂️Husaidia kazi ya tezi koromeo (Thyroid glands)
🧚🏻‍♂️Yanaweka sawa hormone
🧚🏻‍♂️Huzuia kuonekana mzee wakati umri bado (anti aging)

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad