MAFUTA MAZURI YA NYWELE AINA ZOTE

Watu wengi wamekua wakihangaika kutafuta mafuta mazuri yatakayoweza kukuza nywele zao kiusahihi na bila madhara yoyote, lakini wengi wamekua wakiangukia katika mikono ya watu ambao hawana ujuzi wa kutosha kuhusu mafuta na matunzo ya nywele in general, kwa hiyo wamekua wakipata mafuta yenye kemikali kali au mafuta makali; kitu ambacho kinawapelekea kutopata matokeo ambayo wanayataka au matokeo wanayoyataka yakachelewa sana.

Sasa leo tuomgelee mafuta ya aina tatu ambayo ni Natural, mazuri sana kwa nywele za aina yote na yatakupa matokeo mazuri ndani ya muda mfupi.

AINA YA KWANZA: MAFUTA YA PARACHICHI (AVOCADO OIL)


Mafuta ya Parachichi yana virutubisho vingi sana kama vile Vitamin A, B, D na E, Protein, Iron (madini chuma), Magnessium, nk ambavyo husaidia sana katika kukuza nywele. Mafuta ya parachichi pia hurekebisha nywele zilizokatika, yanalainishabna kung’arisha nywele na pia hulinda nywele dhidi ya miale mikali, kudhurika na kuungua na jua kali.
NB: Unaweza kuchanganya mafuta ya parachichi kidogo na shampoo wakati unaosha nywele zako ili kuzuia nywele kuwa kavu na kuretain mafuta ya asili (natural oil) kwenye nywele.

AINA YA PILI: MAFUTA YA MNYONYO (CASTOR OIL)
Mafuta haya yana virutubisho vingi pia kama vile vitamin E, protein kwa wingi nk ambavyo husaidia kukuza nywele vizuri zaidi na kuziepusha na kukatika katika. Haya ni mafuta mazuri sana ambayo yanatumiwa kwa nywele za aina zote, yana faida nyingi sana ikiwemo:
🧚🏻‍♂️Kuondoa mba kichwani
🧚🏻‍♂️Kuondoa miwasho
🧚🏻‍♂️Kuponya vidonda, mapunye na magonjwa yote ya ngozi kichwani
🧚🏻‍♂️Yanakuza nywele kwa haraka 
🧚🏻‍♂️Huzuia nywele kukatika na kuzipa nywele unyevu unyevu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad