UTUNZAJI SAHIHI NA BORA WA NYWELE

Leo tuangalie tips mbalimbali zitakazokusaidia kutunza nywele vizuri na kwa usahihi, ila kuwa na nywele nzuri sana na za kuvutia.

JINSI YA KUTUNZA NYWELE ZILIZOSUKWA
-Kusuka nywele style yoyote kuna tegemea na uwezo na aina ya  nywele zako;  kama una nywele  laini sana usisuke style za kubana na kizivuta sana  nywele zitakatika sana.
-Kabla ya kusuka nywele fanya STEAMING ili nywele zako ziwe na proteins muda wote utakaokua umesuka.
-Kama ngozi yako ya kichwa ni   kavu sana ambayo inanyonya mafuta kwa haraka; basi jitahidi sana kufanya hot oil treatment  kila siku ya kuosha nywele (WASH DAY) hii husaidia sana  kuhifadhi natural oils na kuipa ngozi ya kichwa na nywele unyevu kipindi ambacho nywele zinasukwa
-Usifumue na kusuka style nyingne hapo hapo ziache nywele zipumue kwa muda kidogo  halafu usuke tena, hapa waweza fanya "PROTECTIVE STYLES  TU”  kama twists au mabutu ya kawaida
-Usisuke nywele zako zikiwa chafu bali suka nywele zilizo safi, ambazo zimefannyiwa treatment na ambazo zina unyevu wa kutosha. 
-Andaa mafuta ya kukuza nywele BLACK CASTOR OIL  inashauriwa zaidi sababu ina unyevu wa kutosha na chakula chenye kuleta afya bora kwa nywele yako kipindi chote utakachokua umesuka kua unapaka mafuta nywele isikauke na pia kwaajili ya massage katika ngozi ya kichwa chako.
-SPRAY BOTTLE  ni muhimu sana kwa kuzipa unyevu nywele zako muda wote. 
-Usikae na nywele muda  mrefu maana zikikaa muda sana nywele itakua dhaifu na ukifumua utaona inatoka hivyo usipemdelee kukaa na nywele muda mrefu  sana
-Ukilala usiku lala na kofia au kitambaa cha SATINI ambayo ni muhimu sana, satin inasaidia sana kuzuia kukausha mafuta na pia mto usinyonye mafuta.
-Jiepushe  kukaa kichwa wazi kwenye jua kali, miale ya jua huharibu virutubisho na kukausha unyevu unaolinda nywele isiwe kavu na kusababisha ukavu mwishowe kukatika kwa nywele
-Ukiwa umesuka jiepushe na vumbi au uchafu wa aina yoyote ili nywele yako isipate uchafu ukiacha ipate vumbi nywele itaanza kuwasha wakati imesuka
-Hakikisha unamwambia msusi wako asiguse zile nywele za mbele zitakatika na huishia kukosa nywele za pemben kabisa/EDGES

NB: Jitahidi sana kufuata hizi hatua, jitahidi sana kunywa mani mengi, kula mlo kamili, kupunguza stress na kufanya kila kitu ambacho nywele zako zinahitaji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad