MAKOSA YATAKAYOFANYA NYWELE ZAKO ZISIKUE HARAKA

Katika utumzaji wa nywele haswa nywele asilia, watu wengi hufanya vitu ambavyo wanaamini ni sahihi lakini kwa upande mwingine huwa sio sahihi. Leo tuangalie baadhi ya makosa ambayo mtu anaweza kufanya yakapelekea nywele zake kudumaa na hivyo kutokukua vizuri. Baadhi ya makosa hayo ni;
🧚🏻‍♂️ Kublowdry au wananyoosha nywele  mara kwa mara. Mtu akifanya hivi basi, ataziua nywele zake na zitaanza kukatika wakati wa kuchana au muda wowote. Hivyo kama unataka nywele zako kukua vzr inabidi upunguze kutumia vifaa kama hivi ili nywele zako zikue ( Hata kama umepaka dawa)
🧚🏻‍♂️Jinsi  nywele zinavoachiwa  na kuzistyle au kusuka  rasta, nywele za kawaida au kushonea weaving zinakubalika, ila ukizichana na kuzibana  nywele basi hapo inaweza kuziharibu au kuzikata nywele. Hivyo inatakiwa kuwa makini sana kwenye mitindo na styles za nywele zetu
🧚🏻‍♂️Kutokata  ncha baada ya muda, ncha zinaweza kuanza kuchanika na inabidi uzikate ili nywele zikue vizuri kwasababu ncha huchangia kwenye kusitisha ukuaji wa nywele na kukata nywele. Unaweza kukata incha1-2 au cm 2-2.5 baada ya miezi mitatu au minne.
Baaada ya kuona makosa yanayofanyika; Sasa tuangalie jinsi ya kukabiliana nayo.
MBINU ZA KUKUZA NYWELE HARAKA
🧚🏻‍♂️Inatakiwa kusuka  nywele zako mara kwa mara ilizisiharibike au zisikatike. Hivi utaweza hata kuzuia ncha zilizoharibika. Kama hujisikii kusuka nywele au kushonea weaving basi unaweza kuzibana kwa juu au kuzifunga na kitambaa ila ni lazima kitambaa kiwe cha silk ili nywele zako zisiharibike ( unaweza kukitumia hata wakati wa kulala)
🧚🏻‍♂️Inatakiwa  kupaka mafuta kwenye kichwa chako mara kwa mara, sana sana unapojisikia kama kichwa kimekauka au kama kinawasha. Mafuta mazuri kutumia kwa ajili  ya ukuaji wa nywele ni mafuta ya nazi, castor oil,  Moroccan, Jamaican au lavender. Ila hata mafuta mengine yeyote unayotumia ilayasiwe ya mgando
🧚🏻‍♂️Usizioshe  nywele na shampoo mara kwa mara kwasababu shampoo inaondoa mafuta kwenye kichwa na nywele zako. Basi, inabidi uoshe nywele na conditioner kama unaona nywele zako sio chafu sana, ila kama unaona nywele zako ni chafu basi osha na shampoo. Itakuwa bora ukipaka mafuta kabla ujaosha nywele na shampu na uoshe nywele zako kila baada ya wiki moja na kama zinakatika basi, osha baada ya wiki mbili au tatu.
🧚🏻‍♂️Kula  vyakula vingi vyenye protein kama kuku, mtindi, maharagwe au nyama yoyote.
🧚🏻‍♂️Kunywa maji ya kutosha.
NB: NYWELE NZURI AU NGOZI NZURI INATEGEMEA SANA MTINDO WAKO WA MAISHA (Life style)
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad