MAHITAJI
🧚♀️Parachichi 1 kubwa
🧚♀️Ndizi moja iliyoiva vizuri
🧚♀️Yai 1 la kienyeji
🧚🏻♂️Asali kijiko kimoja
🧚🏻♂️Mafuta (Castor oil, jojoba oil or coconut oil) kijiko kimoja
JINSI YA KUANDAA
-Andaa ndizi na parachichi vizuri kisha weka kwneye blender
-Saga vizor mpaka zilainike vizuri kuepuka kubaki na particles kichwani
-Ongeza asali, mafuta pamoja na yai kisha blend tena vizuri
-Baada ya hapo osha nywele zako vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Kausha nywele kidogo kuondoa maji yanayotiririka kisha paka steaming yako kuanzia chini kabisa ya nywele (kwenye shina) hadi juu
-Hakikisha nywele zote zimepata steaming
-Vaa kofia ya plastic (zile za kuogea) kwa dakika 45 au kaa kwenye steamer kwa dakika 20 tu. Hii inafanyika kuongeza joto ili steaming iweze kuingia vizuri kwenye nywele.
-Baada ya hapo osha vizuri na maji ya baridi (kufunga vitundu vilivyofunguliwa na joto)
-Halafu utaendelea na LOC Method kama kawaida
FAIDA ZA STEAMING HII
-Kulainisha nywele na kuzuia zisijifunge funge
-Kung’arisha nywele
-Ni chakula cha nywele hivyo kufanya nywele kukua vizuri
-Kuondoa mba, miwasho nk kwa sababu ya asali ambayo ni antifungus.
NB: Kwa matokeo mazuri fanya hii mara mbili kwa mwezi🔥🔥🔥
NYWELE NZURI NI MATUNZO