MAKOSA UNAYOFANYA WAKATI WA KUOSHA NYWELE ZAKO-PART 1


Leo utajifunza namna sahihi ya kuosha nywele ili uziache nywele zako zikiwa safi kana kwamba umeziosha kwa mtaalamu wa saluni. 
Wote  tunaosha nywele ila haitakushangaza ukisikia kwamba uoshaji wa nywele zako si sahihi. Wengi wetu tumekuwa tukifanya makosa kadhaa wakati wa kuosha nywele. Baadhi yetu hatutumii muda wa kutosha kusugua scrub” ngozi ya kichwa “scalp”, hatuoshi vizuri na baadhi pia hatutumii conditioner. Na haya ni baadhi tu ya mambo ambayo tunakosea wakati wa kuosha nywele.

Yafuatayo ni makosa makubwa matano watu wengi huyafanya wakiwa wanaosha nywele
🧚🏻‍♂️Kutolowanisha nywele vizuri.
Watu wengi hawaloweshi nywele zao vizuri kabla ya kupaka shampoo. Ni muhimu kulowesha kila unywele kwa maji kabla ya kupaka shampoo. Kila nywele inahitaji kuloweshwa, kisha ipakwe shampoo ili ipate kutakata vizuri.
🧚🏻‍♂️Kutumia shampoo nyingi sana au kidogo sana.
Wote  tunafahamu kwamba kitu chochote kikizidi kina madhara au hakitaleta matokeo mazuri. Tunatakiwa kutumia kila kitu kwa kiasi. Si kwa wingi sana na si kwa uchache sana. Kanuni hii pia inatumika kwenye upimaji wa kiasi cha shampoo cha kutumia wakati wa kuosha nywele.
Kutumia shampoo nyingi kunaweza kukufanya usiweze kuipata nywele na kuisafisha vizuri kutokana na kuzidiwa na povu jingi sana. Na kutumia shampoo kidogo kutafanya nywele zako zisitakate vizuri. Pima shampoo kiganjani kwako, kiasi cha wastani kulingana na ukubwa na wingi wa nywele zako, kwa kutumia vidole paka shampoo kwenye nywele zako ulizozigawanya kwenye makundi manne. Paka kuanzia kwenye ngozi ya kichwa “scalp” kuja kwenye ncha ya nywele
🧚🏻‍♂️Kutotilia  maanani zaidi ngozi ya kichwa.
Kama  umeshawahi kufanyiwa shampoo kitaalam saluni bila shaka unajua ni muda kiasi gani huwa wanautumia kwenye ngozi ya kichwa. Kusugua ngozi ya kichwa ni hatua ya msingi zaidi kwenye mchakato wa kuosha nywele.
Watu wengi hawatumii muda wa kutosha kusugua ngozi zao za kichwa. Tunatakiwa kusugua ngozi zetu za kichwa kwa walau dakika tatu. Bila kujali urefu au aina ya nywele zako unachotakiwa ni kusugua ngozi yako ya kichwa. Na unatakiwa kufanya hivyo kwa kutumia vidole na sio kucha kwa muda usiopungua dakika tatu.

INAENDELEA....
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad