13. FAIDA ZA TUI LA NAZI KWEYE NYWELE

FAIDA ZA TUI LA NAZI KWEYE NYWELE
Mahitaji
🍃Nazi moja iliyokomaa vizuri
🍃Unga wa pilipili  manga nyeusi
🍃Unga wa mbegu za uwatu (fenugreek)

Jinsi ya kuandaa
🌿Kuna nazi yako vizuri kwa kutumia mbuzi au mashine
🌿Tengeneza tui lako zito kidogo ukitumia nazi uliyokuna

NB: Ili kupata tui zito na jingi nakushauri ukisha kuna nazi yako iweke kwenye blender na maji kidogo kwa mbali kisha blend kwa dakika kadhaa ndipo ukamuwe upate tui zito kabisa na jingi.
🌿Mimina tui hilo kwenye sufuria na uweke kwenye moto kama dakika 3 au 4 kustimulate nutrients kwa kuwa litakaa kwenye nywele muda mfupi
🌿Subiri tui hilo lipowe na mwisho pakaa kichwani kichwa chote au sehemu ambayo nywele zimepotea na uache hivyo kama dakika 20 hadi 30 (kama steaming au protein treatments nyingine)
🌿 Safisha  kichwa na nywele zako kwa kutumia mild  shampoo (Isiyo na sulfate au chumvi au viambata vingine vyote vyenye sumu).

Faida za tui la nazi kwenye nywele
🌿Tui  la nazi lina kiasi kingi cha protein na mafuta mengine muhimu ambavyo huhamasisha ukuaji wa nywele
🌿Husaidia uotaji wa  nywele na hivyo kuzuia kipara  pia.
🌿Tui la nazi likipakwa  mara kwa mara kwenye nywele  halikawii kuleta matokeo mazuri.
🌿Hujaza nywele
🌿Kufanya nywele kuwa nyeusi na kujaa

MUHIMU
 Kufanya tui liwe na nguvu zaidi unaweza kuongeza vitu vifuatavyo;
🌸Kijiko kimoja  cha chai cha unga wa pilipili manga nyeusi
🌸 Kiasi  hicho hicho cha unga wa mbegu za uwatu (Fenugreek)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad