15. TAMBUA AINA YA NYWELE ZAKO NA JINSI YA KUZITUNZA

POROSITY YA NYWELE (HAIR POROSITY)
Kwa kawaida ukiangalia nywele za watu weusi karibia zote zinafanana kwa kuangalia kwa macho ila kwa kiutalam zinatofautiana
Porosity ni uwezo wa nywele kunyonya na kupoteza unyevu na kila mtu ana uwezo wa kutambua nywele zake zina porosity ya aina gani kwa kutumia kipimo rahisi tu.
☘️Kuna watu wanalalamika mbona nywele zangu hazikui au zinakatika wakati natumia mafuta sawa na mtu fulani?.
☘️Sababu ni kwamba nywele zetu zinatofautiana hivyo mafuta fulani yanaweza kukubali nywele za wenzio na yakakataa kwako..
 
🌸Hizo unazoona ndani ya glass ni nywele moja moja. na hivi ndivyo unavyopima porosity ya nywele zako. Hakikisha nywele zako zimeoshwa vizuri hazina mafuta yoyote kisha chukua nywele moja (hata iliyokatika wakati unaosha inafaa cha msingi iwe safi). Iweke kwenye glass ya maji safi kisha subiri kama dakika moja. ukiona imebaki juu kwa muda wote uliosubiri ujue una low porosity ikiwa kati kati ni normal na ikishuka hadi chini ni high.

🍃LOW POROSITY
Inamaanisha nywele zako hazina uwezo mkubwa wa kuingiza/kunyonya unyevu na kutoa kwa haraka. yani unaweza kupaka mafuta yakakaa muda mrefu hata ukitembea kwenye upepo yanakuwa yapo tu. Pia ukiosha nywele zinakawia kulowa haraka (kunyonya maji haraka mpaka usugue kidogo ndio yaingie ndani).

🌸nywele za aina hii zinakuwa zinafungana sana na hazikui haraka kwa sababu ya kutonyonya unyevu wa kutosha. Ni rahisi pia kuweka mba mana mafuta au conditional vinakaa kwa muda mrefu kwenye nywele

🍃JINSI YA KUZITUNZA
🌸Usipake mafuta mazito kwenye nywele na pia conditions (conditioner au leave in conditioners zilizotengenezwa kiwandani) hutakiwi kuweka mara kwa mara. Kama umeosha kwa kutumia co-wash (shampoo yenye conditioner) hakikisha unafunga nywele zako na kofia za plasic au kama una steamer unaweza kuitumia ili ipate joto na kuyeyuka kwa kuweza kupenya kwenye nywele.
🌸Osha nywele zako angalau mara moja kwa week ili kuzifanya zifunguke na kunyonya unyevu kwa haraka(ukiziosha mafuta yaliyoshindwa kupenya yataondoka na zitapumua).

🍃HIGH POROSITY
Hawa nywele zao zinaingiza unyevu na kutoa kwa kiasi kikubwa sana. kama umepaka mafuta zinaonekana zimeng'ara kwa mafuta lakini baada ya muda mfupi unaona tena ni kavu.

🌸SABABU ZA KUWA HIVYO
-Kuweka dawa ya nywele (mara kwa mara au hata kama ni mara chache).
-Kuzifuta nywele mara kwa mara iwe kwa kubana kwa kukaza sana au kusuka misuko inayokaza sana kiasi kwamba ile hali ya kuvutika kwa nywele inalegea(nywele ukivuta inaonekana kama lastic sasa unapozivuta kila siku lastic inalegea
-Nywele zenye high porosity inaonesha kuwa ni dhaifu sana na zinahitaji matunzo ya karibu
-Kutumia moto (blow dryer au dryer ya kawaida) mara kwa mara

🍃JINSI YA KUTUNZA
🌸Paka mafuta mazito (mfano Black castor oil) yanayozifanya zisiwe nyepesi sana na yanayokaa muda mrefu ili yasipotee kwa haraka. Ikiwezekana paka hata mara mbili kwa siku .
🌸Punguza kuzibana au kuzichana nywele kila mara

☘️Hizo nywele kwenye glass hapo ju ni mfano tu wa nywele. Hiyo inaonekana ni nywele moja na ndivyo nywele zetu zilivyo ukiangalia kwa macho huwezi kuzitambua kirahisi kama zinakuwa lakini zinakua. Na pia nywele zimejipangilia kama magamba ya samaki (ukiangalia kwabukaribu utagundua hilo)

🌸Hilo ya kwanza inaonyesha low porosity inaonekana magamba yake yamefunika sana na ndio mana ni vigumu kuingiza na kupoteza unyevu kwa haraka.
🌸Nywele ya pili inaonekana ya kati yani haijajifunga sana wala kubana sana hivyo unyevu unaweza kuingia na kutoka kwa kiasi cha kawaida tu.
🌸Nywele za mwisho ni nywele inayoonekana kama magamba yake yako wazi na ndio mana ni rahisi kuingiza na kupoteza unyevu haraka ( watu mnaoweka relaxer mjue nywele zenu zinafunuka hivyo na ndio mana ni rahisi kukatika).
🍂Kawaida nywele ukivuta inaonekana kama lastic yaani inavutika lakini unapoivuta sana au kuweka relaxer ile lastic inalegea au kuisha kabisa na hapo ndio unazifanya nywele zako ziwe rahisi kukatika

☘️Kama unaweka dawa (relaxer) hakikisha unaretach kila baada ya week 12 (miezi mitatu) kwa nywele ngumu, week 16 (miezi minne) kwa nywele za kawaida na week 24 (miezi 6) kwa nywele nyepesi maana nywele zinazoota kwa muda huo ni inch moja tu au wakati mwingine haifiki hata inch moja na ndio inayotakiwa tu kuwekwa dawa na sio ambazo tayari zina dawa.
☘️Pia punguza moto au acha kabisa kutumia moto kwenye nywele sio kila ukiosha unaenda salon kwenye ma driyer, unaweza kuosha nywele zako
☘️Pia punguza moto au acha kabisa kutumia moto kwenye nywele zako sio kila ukiosha unaenda salon kwenye dryer, unaweza kuosha nywele zako nyumbani kisha unazipaka leave in conditioner na mafuta ya nywele.
☘️Zikaushe na tshirt au taulo la cotton halafu zifunge mabutu ketsho yake zitakua zimekauka fungua mabutu paka mafuta ya nywele na mwisho cream au hair butter (mostly shea butter)-LOC Method kisha chana tayari kwa kusuka au kustyle nywele zako.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unaelezea vizuri mno. I love everything in this App. It is a must have app for any girl or woman��

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad