17. CHANZO, KUZUIA NA KUTIBU CHUNUSI

CHANZO CHA CHUNUSI
🌸UMRI – mtu  anapofikia umri wa kukua s3x  hormones huongezeka na hivyo husababisha utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi

🌸VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi hata Make-ups na Sprays za nywele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi zaidi

🌸CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufanya chunusi kuwa nyingi zaidi.

🌸DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.

🌸MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika chemicals (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.

🌸MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye  hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.

🌸FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia hapa namaanisha kurithisha

🌸HORMONES- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito kupata chunusi.

🌸USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele husababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwilini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi

🌸MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi chemicals kadha hutolewa mwilini ambazo huweza kuchangia au kusababisha chunusi

MAMBO YA KUZINGATIA ILI USIPATE CHUNUSI
🌸Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu chochote kigumu.
🌸Jaribu kutumia Vipodozi au vilainisha ngozi visivyo na mafuta ya mgando
🌸Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso hapa ni kwa wale wenye nywele ndefu
🌸Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
🌸Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali au kitu kigumu
🌸Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
🌸Punguza mawazo

Kumbuka kuwa chunusi zinawezi kutibika kabisa iwapo matibabu yatakuwa sahihi

Pia unapotumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata  miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa( cream au tube)
Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka

Na hapa watu wengi hupenda kutumia vipodozi vyenye kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

Tumia vitu vya asili ili chunusi ziweze kutoka moja kwa moja. Sio unatumia mara moja tu unarudi kuwa zimegoma kutoka

JINSI YA KUONDOA CHUNUSI,MADOADOA,MABAKA NA MAKOVU USONI
Mahitaji
🍃Limao
🍃manjano
🍃Baking powder( baking soda)

JINSI YA KUTUMIA
☘️Chukua mahitaji yako yote na Pima kijiko kimojakimoja then changanya pamoja,
☘️ paka usoni vizuri kwa kuviringisha Kama mduara usipakae kwa kurudi chini
☘️Hakikisha mchanganyiko hauingii machoni.
 ☘️Kaa nusu saa au saa moja nawa  usoni kwa maji ya uvugivugu, tumia ndani ya wiki moja then utupe maendeleo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad