33. JINSI YA KUFANYA NYWELE KUWA NYEUSI, NDEFU NA NGUMU

Ni kwa muda sasa tumekua tukiongelea jinsi ya kulainisha nywele, kufanya ziwe nyingi nk; Leo tuangalie jinsi ya kufanya nywele ziwe nyingi (kuongeza volume) , kuwa nyeusi na zipendeze kwa kutumia vitu vya asili kabisa unavyoweza kuvipata ukiwa nyumbani.

SABABU ZA KUWA NA NYWELE NYEKUNDU NA NYEPESI
🧚🏻‍♂️ Kupaka paka madawa nywele; Hii hupoteza rangi halisi ya nywele ambapo wengine huwa na nywele nyekundu hata  kama zilikuwa nyeusi.
🧚🏻‍♂️Kutumia moto mara kwa mara kama vile kublowdry, kupasi na kunyoosha nywele kwa kutumia moto.

Katika mazingira hayo unaweza kutumia vifuatavyo ili kurudisha volume na rangi halisi ya nywele.
🧚🏻‍♂️Baking soda: Hii inatumika  baada ya kusafisha nywele zako na kuwa safi.
JINSI YA KUANDAA
🍃Pima vijiko vitatu vya chai (vile vidogo) vya  baking soda
🍃 Unachanganya  na maji
🍃 Unachanganya vizuri mchanganyiko wako na unatumia kuoshea au kusuuzia  nywele.
Hii inasaidia sana katika  kuleta rangi halisi ya nywele.

🧚🏻‍♂️Asali  na mafuta ya mzeituni (Olive oil): Hii inasaidia kwa wale ambao wana  tatizo la muwasho au kupata tatizo lolote kichwani huenda nywele zinakatika bila wewe kujua, tumia vitu hivyo vitakuweka sawa.
JINSI YA KUANDAA
🍃Chukua  asali vijiko viwili (au utakayoona inatosha)
🍃Pima na mafuta ya mzeituni nusu kikombe.
🍃Changanya vizuri mchanganyiko wako
🍃Paka vizuri kwenye eneo lenye tatizo
🍃Unaweza kuvaa shower cap au ukaacha ivo ivo
🍃Acha kwa  kwa muda wa dakika 20 hadi 30
🍃Then osha kwa maji ya baridi.
Nikisema sehemu yenye tatizo namaanisha kama nywele zimepukutika au una mba wanaosababisha unajikuna sana nk.

🧚🏻‍♂️Papai:  Hili linasaidia kwa  watu wengi maana wakishaweka  dawa kichwani huwa wana tabia ya kutaka kuzikata ili wazilinganishe huko saloon, lakini steaming hii ya papai ambayo unaweza kuifanya nyumbani kwako ina uwezo wa kuzifanya nywele zako zilingane.
JINSI YA KUANDAA
🍃 Chukua yogurt  kiasi
🍃 Papai  nusu,
🍃Vichanganye kwa  pamoja (au blend kiurahisi zaidi)
🍃 Kisha baada ya hapo paka mchanganyiko huo kwenye nywele zako
🍃Vaa shower cap au steaming cap
🍃Acha kwa  muda wa nusu saa
🍃 Osha  kwa maji ya vuguvugu.

Nywele ndefu kwa ujumla: kuwa na  nywele ndefu
🍃Chukua  yai moja
🍃Mafuta  ya mnyonyo (Black castor oil)  vijiko vitatu
🍃Kijiko  kimoja cha Vinegar
 Changanya  kwa pamoja kisha paka nywele zako acha kwa muda wa dakika 30 kisha osha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad