32. FAHAMU ZAIDI KUHUSU PRODUCTS BUILD UP

FAHAMU ZAIDI KUHUSU PRODUCTS BUILD UP
Apple cider vinegar
Jinsi ya kutumia
🍃Baada ya kuosha nywele na shampoo (nywele zikiwa safi)
🍃Pima  maji nusu lita (500 mls) ongeza vijiko viwili (2 vya chakula) vya ACV
🍃Nyunyiza (spray) mchanganyiko wako kwemye nywele zako hadi kwenye ngozi
🍃Vaa shower cap yako
🍃Acha mchanganyiko ukae kichwani kwa dk 20 hadi 30
🍃Osha nywele kwa maji mengi (bila shampoo)
NB: Baada ya hapo utaona nywele zinavokua soft lakini zitakua kavu kiasi kwa sababu uchafu wote umetoka kwenye nywele
🍃Baada ya hapo fanya hot oil treatment
🍃Vaa showercap na funika kichwa kwa dk 20 hadi 30 tena
🍃Baada ya hapo osha na shampoo kidogo sana kuondoa mafuta ya ziada
🍃Then paka leave in conditioner na mafuta kidogo halaf unaweza suka any protectibe style au kubana.

NJIA NYINGINE
🍃Osha nywele zako kwa shampoo na hakikisha nywele ni safi kabisa
🍃Changanya maji nusu lita, ACV vijiko 2 na mafuta kidogo (vijiko viwili)
🍃Paka kwenye nywele mchanganyiko wote
🍃Funika kichwa kwa dk 20 hadi 30
🍃Osha na maji mengi
🍃Kama unafanya steaming pia siku hiyo hiyo  muda wa kuweka
🍃Then hatua nyingine zinafuata baada ya kuweka steaming

Limao na Asali
🌸Osha nywele zako na maji ya uvuguvugu ili kufungua matumdu ya kichwa
🌸Pima asali vijiko viwili hadi vitatu (inategemea na uwingi wa nywele zako)
🌸Weka kwenye bakuli safi
🌸kamulia limao nusu (usiweke limao nyingi)
🌸Unaweza kuweka kwenye applicator bottle then paka kuanzia kwenye scalp then massage hadi kwa juu
🌸Vaa showe cap, funika kichwa kwa muda wa dk 20 hadi 30
🌸Osha kwa maji mengi
🌸Baada ya hapo unaweza fuata ratiba yako kama ni steaming au kama ndio umemaliza unapaka leave in conditioner then mafuta then protective style au kubana

Baking soda
🍃Hii inapimwa vijiko viwili vya chakula unachanganya na maji nusu lita then process zote zinaendelea kama za ACV.

NB: Hizi zote zinafanywa mara moja tu kwa mwezi, unaweza jaribu zote then ukachagua inayofanya kazi zaidi kwenye nywele zako.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad