JINSI YA KUFANYA NYWELE KUWA NYEUSI

Nywele nzuri ni matunzo na matunzo hayo yanajumuisha routines mbalimbali za kutunza nywele, kama kuosha nywele, kufanya steaming (steaming ya kawaida na Protein treatment), kuzipa nywele unyevu. Hivyo pale kimoja kinapopuuziwa lazima nywele zisikue vzr na kutokua na rangi nzuri ya kuvutia (NYEUSI); kitu ambacho kinawakera watu wengi sana. Leo tuangalie sababu kadhaa ambazo zinafanya nywele isiwe nyeusi na ya kuvutia.
🧚🏻‍♂️Kutopata mlo kamili na kutokunywa maji ya kutosha
🧚🏻‍♂️Nywele kukosa matunzo stahiki
🧚🏻‍♂️Kutumia bidhaa zisizofaa kwa nywele zako (bidhaa zinatumika kulingana na hair type)
🧚🏻‍♂️Msongo wa mawazo
🧚🏻‍♂️Kutumia dawa zenye kemikali kali (Relaxer)

Hayo hufanya nywele kukosa ule mvuto wake wa asili kabisa na kutopendeza, hivyo kuwakosesha  raha watu wengi sana wanaozingatia muonekano mzuri wa nywele zao.

Leo tuangalie procedure nyepesi tu inayoweza kuurudiaha muonekano wa nywele zao ndani ya muda mfupi sana, zikawa nyeusi na za kuvutia.

MAHITAJI
🧚🏻‍♂️Tui la nazi
🧚🏻‍♂️Mafuta kijiko kimoja (Black Castor oil, Coconut oil or Jojoba oil)

JINSI YA KUFANYA
🧚🏻‍♂️Chukua nazi iliyokomaa vizuri, kisha ikune kwa utaratibu ili utoe vipande vidogo vidogo na kuifanya iwe laini au unaweza tumia mbuzi au Coconut blender kukwangua nazinyako.
🧚🏻‍♂️ Weka maji kidogo na uchuje tui katika chombo kisafi, hakikisha unapata tui la kwanza likiwa zito kabla halijakatika.
🧚🏻‍♂️Osha nywele zako kwa maji safi yenye uvuguvugu mpaka uhakikishe hakuna mafuta wala uchafu ulioganda kwenye ngozi ya kichwa.
🧚🏻‍♂️Baada ya kufuta maji yote kichwani, chukua tui lako la nazi, anza kupaka kwa kuchambua nywele kidogo kidogo hadi uhakikishe zote zimekolea vizuri.
🧚🏻‍♂️Vaa kofia ya plastic au ingia kwenye steamer  au mfuko kwa muda wa saa moja kuliacha tui la nazi lifanye kazi vizuri kichwani. 
🧚🏻‍♂️Baada  ya hapo, osha nywele zako, kausha na upake mafuta mazuri kwa ajili ya nywele.


NB: Ukifanya  hivi kila wiki  nywele zako  zitaimarika na kuwa na afya kwa haraka zaidi. Njia hii inaweza kuwa rahisi kuliko zote kutokana na unafuu wake na upatikanaji wa nazi kwa kuwa kila mmoja anaweza kupata.

ITAENDELEA....
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad