-Vijiko vinne vya chakula vya hena
-Nusu kikombe cha chai ya rangi iliyokolea majani
-kijiko kimoja cha chakula cha juice ya limao
-maziwa ya mgando (yogurt/mtindi)
JINSI YA KUTUMIA
•Osha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo isiyo na viambata sumu
•Kausha nywele zako kidogo ili kuondoa maji yanayochuruzika
•Changanya vitu vyako vyote pamoja
•Paka mchanganyiko huo kichwani
•Kaa nao angalau lisaa.
•Baada ya hapo osha nywele zako na maji ya kawaida mengi
•Halafu unaweza fuata LOC Method kama kawaida.
Hii treatment italainisha nywele kwa maana ya kuzinyoosha na kuzipa mng'ao mzuri.