JINSI YA KUZUIA NYWELE ZAKO KUKATIKA

Henna ina matumizi mengi sana; leo tuangalie jinsi gani unaweza tumia henna kwa matokeo mazuri zaidi.
Leo tuangalie jinsi gani unaweza kutumia henna kuzuia nywele kukatika hasa ncha.

MAHITAJI
Vijiko vi 2-3 vya chakula vya henna
•Parachichi moja la wastani
•Yai moja (La kienyeji)
•Maji kidogo kama mchanganyiko utakua mzito sana

JINSI YA KUTUMIA
-Osha nywele zako vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Kausha kidogo nywele zako kuondoa maji yanayochuruzika
-Changanya vitu vyote upate uji mzito wastani, -Paka kichwani kuanzia kwenye ngozi mpaka ncha ya nywele zako. -Kaa na mchanganyiko huo angalau masaa mawili kisha osha.

KUJAZA NYWELE NA KUFANYA ZING’AE
MAJITAJI
•Chai ya rangi nusu kikombe
•Maji ya limao Kijiko cha chakula kimoja
•Yai au maziwa ya mgado

JINSI YA KUTUMIA
Loweka Henna usiku mzima kwenye chai ya rangi. asubuhi unapotaka kutumia ongezea viungo vilivyobakia. Paka dakika ishirini (20) Kabla ya kuoshwa nywele.

HENNA KWA AJILI YA NYWELE KAVU
Changanya Henna, mafuta ya nazi kiasi na Olive oil (mafuta ya mzaituni) uwe na uji mzito kiasi. Paka kichwani kaa nao lisaa kisha safisha.

NB: Hizi  treatment unaweza kufanya kwa nywele natural na zinye dawa, hakikisha unatumia Henna ya asili isiyotiwa kemikali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad