JINSI YA KUKUZA NYWELE KIRAHISI

Leo tuangalie mtu anawezaje kukuza nywele zake za asili kirahisi kabisa kwa kutumia vitu vya kawaida ambavyo vinapatikana jikoni kwa kila mtu.

MAHITAJI
-Kitunguu maji
-Tangawizi
-Kiazi mviringo
-Olive oil (Mafuta ya mzeituni)
-Mafuta ya nazi (Cococnut oil)
-Mafuta ya mnyonyo (Black Castor oil)
-Asali kidogo
-Kiazi mviringo

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo husaidia kukuza nywele na kuzuia MBA kwenye nywele.

JINSI YA KUANDAA
 -Chukua kikwaruzio cha nyanya / karoti (grater) halafu chukua  kitunguu chako kwaruza pale upate ule uji uji wake
-Chukua tena tangawizi na kiazi kwaruza/kwangua upate ule uji uji baada ya hapo chukua chujio au kitambaa kisafi changanya huo mchanganyiko wako wote then chuja/kamua ili kupata juice  yake
-Ongeza vingine vyote vilivyobaki na uchanganye vizuri (mafuta unaweza kidogo kidogo tu)

NB: Unaweza kutumia blender kusaga vitu vyako vyote kwa pamoja halafu mwisho utachuja upate maji maji yake

JINSI YA KUTUMIA HUO MCHANGANYIKO WAKO
-Chukua chupa  weka hiyo juice iliyopatikana
-Funua nywele zako na uzipshe vizuri na shampoo isiyo na viambata sumu
-Paka  huo mchanganyiko wako kweny ngozi ya kichwa kwa kutumia vidole na sio kutumia kucha  paka kichwa mpaka kienee chote
-Chukua mfuko wa plastic au makofia   ya plastic vaa kichwan kwa muda wa saa moja au unaweza kulala nayo usiku kucha
(pia unaweza kukaa kwenye steamer kwa dakika 20 hadi 25 ili kupata joto vizuri)
-Baada ya hapo osha nywele zako vizuri na maji ya kawaida tu.

JINSI YA KUTUMIA MAFUTA
-Chukua mafuta ya nazi, ya mnyonyo na mzeituni kiasi kidogo changanya alafu yapashe kidogo yapate joto (Hot oil treatment)
- Paka vizur kwenye nywele kuanzia kwenye ngozi ya kichwa halafu kaa  lisaa limoja halafu osha  kwa kutumia shampoo hakika utazifurahia nywele zako.
-Mwisho paka mafuta yako ya joto la kawaida na hapo uko tayari kubana style yoyote au kwenda kusuka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad