JINSI YA KUTUNZA NYWELE ZENYE DAWA



Mara nyingi tumekua tukiongelea nywele za asili (Natural hair) lakini sio watu wote wenye passion (uvumilivu wa kutunza nywele za asili). Hivyo basi leo nitatoa tips kidogo kuhusiana na jinsi ya kutunza nywele zenye dawa (Relaxed hair) ili ziweze kupendeza vizuri.

Nywele zenye dawa ni nywele ambazo mwanzo zilikua za asili lakini zikaongezewa vilainishi (relaxers), hivyo kurudi kuwa natural kutoka kwenye nywele za dawa ni either ufanye transition (kuacha nywele ziotee huku ukipunguza zenye dawa juu) au kufanya big chop (kunyoa kabisa nywele zote na kuanza upya).

Tuangalie vitu vya msingi vya kuzingatia ili uwe na nywele nzuri zenye dawa
🧚🏻‍♂️Hakikisha unachagua dawa ya nywele inayoendana na nywele zako. Hapa pemdelea sana kutumia dawa za box na sio za kopo maana dawa za kopo ni kali mno zinaweza kuleta madhara ndani na nje ya kichwa ndani ya muda mfupi. Na dawa za nywele zinawekwa chini tutu kwenye maotea ya nywele usiweke juu.

🧚🏻‍♂️Lazima  upange muda wa kuweka nywele dawa. Dawa inatakiwa kuwekwa mara tatu au mbili tu kwa mwaka. Kama nywele zako ni laini basi unaweka kila baada ya miezi 6 na kama nywele zako ni ngumu sana basi kila baada ya miezi minne ndio unaweka dawa. Usiweke mara kwa mara; kumbuka hizo ni chemicals na zinaenda kukutana na ngozi ya kichwa directly. Pian wengine huweka dawa baada ya miezi mitatu vyote inategemea na aina ya nywele zako.

🧚🏻‍♂️Suka  mitindo rafiki na nywele zako usipende kusuka tu kila mtindo chagua mitindo ambayo haitakata nywele zako.

🧚🏻‍♂️Hakikisha  unaosha nywele zako mara  kwa mara. Angalau  mara  3 au nne kwa mwezi. Nywele zikijaa uchafu haziwezi kupumua vizuri hivyo zitakua kwa kusua sua sana.

🧚🏻‍♂️Tumia  mafuta rafiki na nywele zako. Mafuta  yenye uwezo wa kutunza unywevu na kuzuia nywele kukatika. Mafuta hayo ni kama vile Black castor oil, Coconut oil, Olive oil, jojoba oil nk

🧚🏻‍♂️Punguza  matumizi ya moto kwenye nywele..  Mfano .kupasi nywele au kukausha nywele na dryer. .Hii  hufanya nywele kutokuwa na nguvu hivyo kuwa dhaifu sana hivyo unashauriwa usifanye mara kwa mara.

🧚🏻‍♂️Tumia kofia ya satini au kitambaa cha safini wakati wa kulala (usilale kichwa wazi au na kitambaa kigumu); Hii inasaidia  nywele kufyonza mafuta ipasavyo na  kumaintain Ph
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad