31. FAHAMU ZAIDI KUHUSU PRODUCT BUILD UP

FAHAMU ZAIDI KUHUSU PRODUCT BUILD UP
Product build up kwa kiswahili chepesi ni uchafu uliojilundika kichwani ambao hauwezi kuondolewa kirahisi kwa kutumia shampoo wala conditioner ya kawaida. Mtu anaweza kuwa anaosha nywele kila wiki au hata mara mbili kwa wiki lakini bado kukawa na product build up, labda awe anatumia clarifying shampoo ambayo inaondoa kila kitu kwenye nywele pamoja na mafuta ya asili kichwani. In short ni uchafu mgumu sana kutoka.

Product build up ni uchafu unaotokana na products unazipaka kila mara mfano unachanganya changanya mafuta, unapaka conditioner yoyote (muda mwingine hata haiendani na nywele zako), shampoo zenye sulfates/chumvi na viambata sumu, lotions za nywele, creams na gels za kila aina. Pia inatokea hata kama unatumia products sahihi ni vile lazima kiwango flani kibaki kwenye nywele.

MADHARA YA PRODUCT BUILD UP
🍃Zinaziba hair pores
🍃Ukavu uliokithiri kwenye nywele (unaweza kuwa unamoisture nywele na maji kila siku lakini bado nywele ni kavu)
🍃Nywele kutokuleta matokeo unayotaka (Unaweza kuwa unafanya steaming mara kwa mara lakini bado nywele zinakakamaa na kuwa kavu)
🍃Hakuna kitu kinachoingia ndani ya nywele zako
🍃Nywele hazijibu jitihada yoyote unayofanya
🍃Nywele kuwa ngumu continuously (unaweza tumia mafuta ya kila aina lakini nywele bado ngumu tu).
🍃Nywele inaweza kuwa inaonekana ina mafuta kwa nje lakini kwa ndani kavu na huwezi ata kuivuta
🍃Nywele kukatika zaidi kwa sababu ya ukavu

VITU VINAVYOONDOA  PRODUCTS BUILD UP
1. Apple cider vinegar with the mother
Umuhimu wake
-ACV ina uwezo wa kuondoa uchafu wote kwenye nywele (clarifying properties) pamoja na kufungua vitundu kwenye ngozi ya kichwa.
-Ina uwezo wa kuondoa fungus pamoja bacteria wote kwenye nywele hivyo inapunguza maradhi kwenye ngozi ya kichwa, ukavu, kuwashwa pamoja na mba.
NB: Tumia Apple cider vinegar with the mother hii ndio ACV natural, usitumie ile ya American garden.

2. Limao/ndimu na asali
Umuhimu wake
-Hii pia inaondoa fungus, bacteria na  mba pia kwa sababu ya uwepo wa citric acid kwenye limao au ndimu hivyo kuondoa products build up kwa ufanisi zaidi.


3. Baking soda
Umuhimu wake
-Hii  ni alkali hivyo inauwezo wa kucleanse au kusafisha sana ngozi ya kichwa na hivyo kuondoa products build up zote.
NB: Baking soda inayotumika hapa ni ile ya blue (chapa  simba) au ukipata hii ni nzuri zaidi.
INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad